Mapishi (7)
.jpg)
-
Mimina unga, samli na chumvi kwenye sinia au bakuli kubwa. Changanya pamoja.
-
Mimina maji kidogo kidogo huku unachanganya na ule mchanganyiko wa unga.
-
Mchanganyiko ukishashikana, kanda unga kwa mkono kiasi, kama dakika tano
-
Funika na uache mchanganyiko kwenye sinia kama dakika kumi hivi kwa kuufunika ili hewa isiingie.
-
Gawanya ule mchanganyiko kwa kufanya madonge kama kumi na nne au kumi na sita kwa chapati ndogo.
-
Mimina unga kidogo mahali ambapo utasukuma chapati.
-
Sukuma donge moja mpaka liwe duwara jembamba.
-
Paka samli kama kijiko kimoja cha kulia, ukihakikisha umepaka duwara lote.
-
9. Kunja lile duwara kama mfano wa kamba, huku unazungusha kama kamba ili iwe ndefu kidogo.
-
Zungusha ile kamba iwe mviringo. Funika na kitambaa kisafi cha jikoni ambacho kimajimaji kidogo.
-
Endelea namna hii mpaka umalize madonge yote.
-
Sukuma chapati iwe mviringo kama nchi 7 hivi
-
Pika chapati kwenye frying pan moto wa kiasi. Ikiiva upande mmoja na kuanza kufura/kuvimba, geuza upande wa pili. Tumia kitambaa kisafi cha jikoni kugandamizia na kuzungusha zungusha ile chapati. Ikiiva upande wa pili, mimina kijiko kimoja cha kulia cha samli na ugeuze chapati tena, zungusha zungusha kisha mimina nusu kijiko cha kulia cha samli na ugeuze upande wa pili kidogo. Toa chapati uweke kwenye sahani. Ikunje kunje kidogo kisha uifungue vizuri.
-
Endelea namna hii huku unafuta frying pan na kitambaa kisafi au karatasi za jikoni (tissue) baada ya kila chapati.
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)

-
Ikiwa mbaazi sio za tayari, loweka uchemshe hadi ziive.
-
Osha vizuri mchicha kisha, katakata mdogo mdogo (chopped) au tumia ulio tayari wa barafu (frozen chopped spinach)
-
Katika sufuria, tia mchicha pamoja na mbaazi zilizokwisha iva.
-
Katakata kitunguu, utie humo, tia nyanya kopo, tia chumvi na pilipili mbichi nzima .
-
Tia tui upike katika moto mdogo mdogo hadi zitokote na kuiva mchicha, usiache zikauke sana. Tayari kuliwa na chapati, maandazi au wali.

-
Osha mbaazi kwenye chungio na ziache zitoke maji.
-
Kaanga kitunguu kidogo tu kisha tia mbaazi na majano.
-
Tia kidonge cha supu na chumvi pilipili mbichi na nazi
-
vikombe vitatu, utabakisha nusu kikombe.
-
Ikisha kauka kidogo changanya nazi ya unga kama
- Vijiko 4 vya supu kwenye nazi uliobakisha, mimina kwenye mbaazi
-
Iache motoni kidogo hadi iwe nzito na itakuwa tayari kuliwa kwa maandazi au chapati.

-
Chemsha kunde kavu bila ya kuloweka kwa maji vikombe 4 na sukari kikombe kimoja kwa moto kiasi mpaka ziive
-
Kisha mimina vitu vyote vilivyobakia pamoja na maji vikombe 3 vilivyobaki na acha ichemke taratibu mpaka maji yapunguke uji uwe mzito.
-
Epua mimina kwenye bakuli na tayari kwa kuliwa.

Namna ya kutayarisha-
Katakata vitu vyote vipande weka katika bakuli
-
Tia katika mashine ya kukamua juisi, washa mashine ikamue juisi.
-
Mimina katika gilasi ikiwa tayari kunyiwa
.jpg)
-
Pilau ya Sosi ya Soya na Mboga

-
Tia mafuta ndani ya karai. Yakipata moto kiasi, mimina vitunguu maji na mdalasini 1 mzima kaanga. Itachukua muda kidogo. Kaanga mpaka viive viwe rangi ya hudhurungi (brown). Viepue na uweke kando.
-
Ndani ya sufuria kubwa, mimina kuku, chumvi, thomu (kitunguu thomu) na tangawizi, sosi ya soya, pilipili manga, pilipili mbichi, chemsha mpaka kuku aive na maji yakauke.
-
Changanya vitunguu ulivyokaanga, kabichi, pilipili, mboga, kotmiri, mchanganyiko wa mboga za barafu na weka kwa muda wa dakika tano au kumi. Tia na mafuta kidogo uliyokaangia vitunguu .
-
Chemsha mchele na chumvi uive kama kawaida ya kupika wali wa kuchuja (wali wa maji). Ukishauchuja umwagie katika masala ya kuku.
-
Nyunyizia mafuta kidogo uliokaangia vitunguu.
-
Weka moto mdogo mpaka wali ukishaiva, uchanganye ukiwa tayari kwa kuliwa.
2. Kabaabu za Kuchoma katika Vijiti

-
Saga nyama pamoja na kotmiri mara mbili iwe laini kuliko ya sambusa.
-
Tia kwenye bakuli na changanya na vitu vyote pamoja.
-
Viringisha kwenye vijiti vya kuchomea na acha kama muda wa saa.
-
Choma (bake) katika oven kwa moto wa 350?c mpaka zigeuke rangi na kuiva.
-
Zikishaiva ziweke kwenye sahani tayari kwa kuliwa na saladi, chips, mikate au wali.
-
Ni vema kuloweka vijiti vya kuchomea kwenye maji usiku nzima ili ukichoma kababu vijiti visiungue.
-
Tumia bizari zako mwenyewe upendazo ikiwa huna hiyo ya Shan Chapplin Kabaab Mix.

-
Tia maziwa, shirah ya rozi na barafu katika jagi la kusagia (blender)
-
Saga kwa muda wa dakika moja au mbili.
-
Mimina sharbati kwenye gilasi ikiwa tayari.
Mtoto ale chakula muda gani?
Chai ya asubuhi: Saa 12:00 mpaka 2:00 kutegemeana na ni muda gani mtoto anakwenda shule. Jambo la muhimu ni kuwa, mzazi/mlezi ahakikishe mtoto anakula asubuhi ili asiende shle akiwa na njaa, ikibidi mzazi/mlezi amfungie mtoto chakula abebe.
Chakula cha mchana: Muda wa kati ya saa 5:30 mpaka saa 7:00 mchana.
Chakula cha jioni: Saa 10:00
Chakula cha usiku: Saa 1:00 usiku
Jinsi ya kuandaa chakula cha siku ya Jumatatu
Asubuhi: Kifungua kinywa (Breakfast)
Mlo 1: Chapati Maji Na Juisi Ya Chungwa
Mahitaji: 250 gram Unga wa ngano, 1 yai, 100 gram maziwa ya maji, 20 gram mafuta ya mahindi, 10 gram baking powder
Jinsi ya kuandaa chapati maji: Changanya vitu vyote katika bakuli kisha piga na mchapo mpaka upate mchanganyiko safi na laini kabisa. Iwapo mchanganyiko bado mzito ongeza maji kiasi.
Jinsi ya kuandaa juisi ya chungwa: Menya chungwa safi kabisa ili kuondoa uchungu wa gesi iliyopo katika maganda. Kisha tumia chombo maalumu cha kukamulia juice, kamua kisha hifadhi katika friji bila kuweka sukari ili ikae kwa muda bila kuharibika. Kumbuka pia kuweka sukari wakati wa kunywa.
Mlo 2: Uji wa Ulezi na Mtindi
Mahitaji: 200 gram unga wa ulezi, 100 gram maziwa ya maji, 350 gram maji, 100 gram mtindi usio na ladha ya matunda
Jinsi ya kuandaa uji wa ulzei na mtindi: Changanya unga wa ulezi na maziwa katika bakuli kisha chukua sufuria weka maji kiasi cha gram 350. Chemsha maji yakishachemka weka mchanganyiko wa maziwa na unga wa ulezi koroga mpaka uchemke na kuchanganyika safi kabisa ili uji wako usishike chini na kuungua. Acha uchemke vizuri kisha onja ukipata ladha ya kuiva kwa nafaka utakua tayari.
Toa jikoni weka katika bakuli litakalotumiwa na mtoto kisha changanya mtindi usio na ladha ya matunda pamoja na sukari tayari kwa mtoto kunywa.
Mchana: Chakula cha mchana
Mlo: Glass ya maziwa na mkate wa nyama za kusindika
Jinsi ya kuandaa: Mpatie mtoto 200 gram za maziwa sawa na glasi moja ya uvuguvugu au ya baridi lakini kumbuka yawe yamechemshwa vizuri na yakapoa kwa ajili ya usalama.
Kisha chukua vipande viwili vya mkate paka siagi au mayonaisi. Kisha chukua beef salami na beef backon weka kati kati pamoja na slice ya nyanya na tango mbichi mpatie mtoto ale.
Jioni: Chakula cha jioni
Mlo: Sahani ya mchanganyiko wa mboga mbichi
Jinsi ya kuandaa: Chukua caroti, tango, pilipili hoho nyekundu na ya kijani zote mbichi na zuchini ichemshe kidogo kisha weka mtindi wenye ladha ya matunda kwa ajili ya kulia hizo mboga.
Huu ndio muonekano wa sahani ya mchanganyiko wa mboga kama mtoto ni mdogo sana zisage kwenye mashine ya kusagia nyama kisha utapata mchanganyiko laini mpatie mtoto asiyeweza kutafuna hizo mboga mbichi.
Usiku: Chakula cha usiku
Mlo 1: Supu ya uyoga
Mahitaji: 300gram Uyoga fresh au wa kopo, 50 gram kitunguu maji, 10 gram kitunguu swaumu, 10 gram tangawizi, 50 gram leeks, 100 gram viazi mbatata, 100 gram maziwa fresh, 50 gram mafuta ya kupikia, 300 gram maji
Jinsi ya kuandaa supu ya uyoga: Kaanga katika mafuta ya kupikia vitunguu maji na vitunguu swaumu pamoja na tangawizi. Kisha weka viazi mbatata, leeks na uyoga kaanga tena kiasi kisha weka maziwa na maji acha ichemke mpaka viazi viive kisha toa na saga kwenye blenda. Rudisha jikoni kama itakuwa nzito sana ongeza maziwa au maji kiasi. Usisahau kuweka chumvi kulingana na ladha.
Mlo 2: Kuku maziwa, muhogo na njegere
Mahitaji: 200 gram nyama ya kuku isiyo na mifupa, 100 gram njegere, 200 gram maziwa, 150 mihogo iliyochemshwa kwanza, 300 gram maji
Kulia ni machine ya kusagia nyama utakayoitumia kwa ajili ya kusagia vyakula mbali mbali.
Jinsi ya kuandaa kuku maziwa, muhogo na njegere: Chemsha vyote kwa pamoja kuku na njegere mbichi pamoja na muhogo uliokwisha chemshwa kwanza mpaka ikaribie kukauka mchuzi kisha toa jikoni. Chuja kisha weka mchuzi pembeni.
Chukua mchanganyiko wa njegere, kuku na muhogo. Tumia machine ya kusagia nyama weka huo mchanganyiko kisha saga upate rojo zito kisha rudisha katika sufuri, changanya na ule mchuzi uliochuja ongeza chumvi kulingana na ladha mpe mtoto ale chakula kikiwa cha moto.
Kama huna mashine ya kusagia nyama tumia mwiko kuponda itakua safi kabisa kisha unachanganya na ule mchuzi uliochuja.
Kwa mtoto mkubwa usisage. Baada ya kuchemsha ikaiva ongeza chumvi kisha mpakulie ale chakula cha moto atafurahia sana mchanganyiko wa ladha ya chakula hiki.
Orodha kwa ajili ya manunuzi siku ya Jumatatu
Uyoga wa kopo au fresh, mihogo mibichi, pili pili hoho, tangawizi, unga wa ngano, mayai, maziwa, sukari, chumvi, njegere, nyama ya kuku, tango, zucchini, mtindi usio na ladha ya matunda, mtindi wa ladha ya matunda, baking powder, viazi mbatata, mafuta ya mahindi na leeks.
Vitu hivi vyote sio vingi na unaweza kuvitumia siku inayofuata maana menu yetu ina uwiano safi kabisa. Vitu vingi vinatumika karibu kila siku na manunuzi yake sio ghali kabisa. Mpe mwanao raha kwa kula chakula safi na salama.
Kwa maelezo zaidi, tembelea blog ya www.activechef.blogspot.com ambapo Chef Issa anachambua na kuelezea namna ya kuandaa mapishi mbali mbali kwa ufundi na ubora wa hali ya juu. Kwa mawasiliano, unaweza kumuandikia kupitia email yake ya This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.


.jpg)
.jpg)
.jpg)


.jpg)

Read more...